Bunge Urusi kujadili utaifishaji mali za wapinzani wa vita
20 Januari 2024Spika Vyacheslav amesema Jumamosi kwmaba sheria itawasilishwa bungeni wiki ijayo, kuwanyang'anya mali zao maadui wa taifa la Urusi na wapinzani wa vita nchini Ukraine.
Ilihitajika "kuwaadhibu wahalifu wanaoitupia uchafu nchi yetu, askari na maafisa ambao wanashiriki katika operesheni maalum ya kijeshi," Spika wa Duma aliandika kwenye Telegraph, akitumia neno linalotumiwa na ikulu ya Kremlin kuzungumzia uvamizi wa kijeshi nchini Ukraine, ulioanzishwa Februari 2022.
Alisema sheria husika italetwa katika Duma siku ya Jumatatu.
Sheria hiyo mpya itaruhusu kutaifishwa kwa "fedha, vitu vya thamani na mali nyingine iliyopangwa kutumiwa au kutengwa kwa ajili ya shughuli za uhalifu zinazoelekezwa dhidi ya usalama wa Shirikisho la Urusi," Volodin alisema.
Aliorodhesha shughuli nane ambazo zinaweza kusababisha kunyang'anywa mali, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono vikwazo dhidi ya Urusi.
Sheria kadhaa zimepitishwa tangu uvamizi wa Ukraine karibu miaka miwili iliyopita ili kuwaadhibu wapinzani wa vita na wale wanaoonekana kuipaka matoke sifa ya jeshi.
Soma pia: Wabunge Bunge la Ulaya wataka raia wa Urusi wasaidiwe
Utaifishaji wa mali sasa unaongezwa kwenye adhabu. Watu wanaotoa usaidizi kwa mashirika ya kimataifa ambayo Urusi si mwanachama pia watanyang'anywa mali zao katika siku zijazo.
"Mtu yeyote anayejaribu kuiharibu Urusi au kufanya uhaini, atapata adhabu yao wanayostahili na kufidia uharibifu uliosababishwa kwa nchi kwa mali zao," Volodin alisema.
Wanasiasa walioko uhamishoni sasa wanakabiliwa na kunyang'anywa mali zao. Volodin alitaja hasa wasanii ambao wameipa mgongo Urusi na wanaunga mkono Ukraine.
Sheria lazima iwasilishwe mara tatu katika Duma na Baraza la Shirikisho, ambalo ndiyo baraza la juu la bunge, kabla ya kusainiwa na Rais Vladimir Putin. Mchakato huo unaonekana kama utaratibu wakati Volodin akipendekeza sheria hiyo.
Mamia ya maelfu ya Warusi wameondoka nchini humo tangu kuanza kwa uvamizi wa Ukraine. Raia mashuhuri wamekosoa vita kutokea nje ya nchi, na kwa muda mrefu kumekuwa na mjadala nchini Urusi juu ya jinsi ya kuwashtaki.