1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiBurkina Faso

Burkina Faso kufuta kandarasi za makampuni ya madini

Saleh Mwanamilongo
5 Oktoba 2024

Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso ametangaza kufuta kandarasi za uchimbaji madini kutoka kwa baadhi ya makampuni ya kigeni.

https://p.dw.com/p/4lRrK
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Ibrahim Traore atangaza kufuta kandarasi za uchimbaji madini ya dhahabu
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Ibrahim Traore atangaza kufuta kandarasi za uchimbaji madini ya dhahabuPicha: Donat Sorokin/TASS/dpa/picture alliance

Katika hotuba ya kuadhimisha miaka miwili tangu achukue mamlaka, leo Jumamosi, Traore amesema wanajua jinsi ya kuchimba dhahabu yao na haelewi kwa nini wataendelea kuruhusu makampuni ya kimataifa kuja kuchimba madini hayo. Hata hivyo kiongozi huyo wa kijeshi hakubainisha ni kandarasi zipi zitakazofutwa.

Dhahabu ndiyo bidhaa kuu inayosafirishwa nje ya nchi na Burkina Faso. Makampuni ya madini kutoka Uingereza, Australia, Canada na Urusi yanafanya kazi nchini humo. Lakini shughuli za uchimbaji madini zimetatizika kutokana na ongezeko la ukosefu wa usalama.

Licha ya utawala wa kijeshi kuahidi kukomesha machafuko ya makundi ya kigaidi lakini zaidi ya watu 8,000 waliuliwa mnamo mwaka uliopita.