1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBurkina Faso

Burkina Faso yachunguza vidio ya kukatwa miili ya binaadamu

11 Novemba 2024

Vikosi vya jeshi nchini Burkina Faso vimeanzisha uchunguzi baada ya video iliyosambaa mitandaoni kuonyesha watu waliovalia sare za jeshi wakiukatakata mwili wa binaadamu.

https://p.dw.com/p/4mr7q
Burkina Faso
Serikali ya jeshi la Burkina Faso imeanzisha uchunguzi wa vidio ilyosambaa mitandaoni ikionyesha watu waliovalia sare ya jeshi wakikata mwili wa binadaamuPicha: BURKINA FASO'S PRESIDENTIAL PRESS SERVICE/REUTERS

Utawala wa kijeshi nchini humo umesema wameziomba mamlaka husika kutizama uhalisia na chanzo cha vidio hiyo pamoja na kuwatambua wahusika ili wawajibishwe, ikiwa tukio hilo litathibitishwa.

Vidio hiyo hionyeshi eneo kulikofanyika kitendo hicho, siku wala wahusika, ambao miongoni mwao walikuwa wamevalia sare za jeshi.

Taarifa ya jeshi imesema tukio hilo baya kabisa ni linakwenda kinyume na maadili ya kijeshi.