Burkina Faso yapokea ngano iliyoahidiwa na Urusi
27 Januari 2024Nafaka hiyo ilikuwa imeahidiwa na Putin wakati wa mkutano wa kilele wa Urusi na mataifa hayo ya Afrika yanayozijumuisha Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Eritrea, Somalia na Zambia mjini Saint Petersburg mnamo Julai mwaka jana.
Burkina Faso yasifu hatua ya Urusi ya kupeleka ngano nchini humo
Waziri wa mshikamano na hatua za kibinadamu wa Burkina Faso Nandy Some Diallo, amesema ngano hiyo imeonesha kujitolea kwa Urusi katika kuunga mkono juhudi za mamlaka ya nchi hiyo inayokabiliwa na mzozo wa usalama.
Soma pia:Putin akutana na viongozi wa Afrika
Balozi wa Urusi Alexei Saltykov, amesema ngano hiyo ni ishara kali ya nia ya rais wake ya kutoa msukumo mkubwa kwa ushirikiano na Burkina Faso, mmoja wa washirika wake wa kimkakati barani Afrika.
Soma pia:Putin aipongeza Afrika inavyoshughulikia masuala ya kimataifa
Waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso Karamoko Jean Marie Traore amesema msaada huo unapaswa kusaidia kuishinikiza nchi hiyo kuimarisha uwezo wake wa uzalishaji chakula ili kukomesha mara moja utegemezi wa chakula kutoka nje.