1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burundi: Miaka 15 baada ya vita vya msituni, hali ikoje?

Mwandishi: Amida ISSA -DW,BUJUMBURA15 Novemba 2018

Burundi yaadhimisha siku ya wapiganaji. Maadhimisho haya yalioandaliwa na chama Cndd Fdd yametajwa kama fursa ya kuwakumbuka waliopoteza maisha yao kwenye uwanja wa mapigano wakati wote wa vita hivyo vilodumu miaka 10.

https://p.dw.com/p/38JIu
BUJUMBURA Burundi Präsident Pierre Nkurunziza 1st L Front inspects
Picha: Imago/Xinhua/E. Ngendakumana

Leo ni mwaka wa 15 tangu rais Pierre Nkurunziza kiongozi wa uasi zamani kurejea Burundi baada ya kuendesha vita vya msituni kwa kipindi cha miaka 10. Lakini chama tawala nchini humo Cndd Fdd kilichoendesha vita hivyo kinasema malengo makuu ya kuwaletea wananchi maendeleo hawajaweza kuyakamilisha. 

Ni katika mkoa wa Gitega kati mwa nchi ndipo viongozi wa nchi na maafisa wakuu wa chama wamejumuika kuadhimisha siku ya mpiganaji, ikiwa ni mwaka wa 15 tangu Pierre Nkurunziza kiongozi wa zamani wa waasi kurejea nchini baada ya kusainiwa mkataba wa usitishwaji mapigano.

Maadhimisho haya yalioandaliwa na chama Cndd Fdd yametajwa kama fursa ya kuwakumbuka waliopoteza maisha yao kwenye uwanja wa mapigano wakati wote wa vita hivyo vilodumu miaka 10. Na pia kuthmini hali ya nchi miaka 15 baadaye.

Evariste Ndayishimiye katibu mkuu wa chama Cndd Fdd amesema siku hii ni fursa nzuri yakukumbuka nyakati ngumu walizo pitia ili waweze kujenga mustakabali wa taifa hili. Ameendelea kusema "Kukutana kwetu hapa ni mmoja ya sababu za kukumbuka madhila tulokumbana nayo vitani, ili hata vizazi vijavyo watambuwe kuwa havitakiwi kurejelea madhila hayo. Na pia kukutana kwetu hapo ni fursa ya kujifunza kuishi pamoja kwa amani na mtangamano."

Novemba 15 mwaka 2003 Pierre Nkurunziza kiongozi wa kundi la uasi la Cndd Fdd akiwa pamoja na washirika wake, alirejea nchini kupitia mikoa ya Ruyigi hadi Gitega akitokea Tanzania
Novemba 15 mwaka 2003 Pierre Nkurunziza kiongozi wa kundi la uasi la Cndd Fdd akiwa pamoja na washirika wake, alirejea nchini kupitia mikoa ya Ruyigi hadi Gitega akitokea TanzaniaPicha: DW/A. Niragira

Hata hivyo kiongozi huo wa chama Cndd Fdd ameongeza kuwa malengo yao makuu ya kuwapatishia wananchi maendeleo bado hawajaweza kuyakamilisha. "Tunatakiwa kuendeleza juhudi hadi maendeleo ya wananchi yaweze kupatikana. Tulikuwa na malengo mengi muhimu baadhi yalikamilika huku mengine kama vita dhidi ya umaskini bado safari imesalia ndefu. Vita hivyo haviwezi kufanikiwa pasina kuwepo na mshikamano kama warundi, Nina wasihi kusikuwepo na atakae choka katika vita hivyo."

Baadhi ya raia wameiambia DW ya kuwa mikwaruzano ndani ya chama hicho cha uasi zamani, ni miongoni mwa sababu zilopelekea kutokamilishwa malengo 46 walokuwa wamepania ili maendeleo yaweze kupoatikana nchini hapa.

Novemba 15 mwaka 2003 Pierre Nkurunziza kiongozi wa kundi la uasi la Cndd Fdd akiwa pamoja na washirika wake, alirejea nchini kupitia mikoa ya Ruyigi hadi Gitega akitokea Tanzania, baada ya kusainiwa makubaliano yalomaliza vita kati ya kundi hilo na serikali ya rais pierre Buyoya na baadaye na Domitien Ndayizeye.

Maadhimisho ya siku hii ilobatizwa ya Mpiganaji, yalitanguliwa na wiki nzima ya shughuli mbali mbali zilofanyika katika mikoa yote ya nchi, ambazo zitatamatishwa jumamosi hii.

 

Mhariri: Iddi Ssessanga