Burundi yapiga marufuku huduma za bodaboda mjini Bujumbura
21 Machi 2022Tangu usiku wa manane polisi wanapiga doria kwenye maeneo ya vitongoji vya jiji kuzuwia kusikuwepo na atakayekiuka hatua hiyo. Hali hiyo imesababisha msongamano mkubwa kwenye vituo vya mabasi, huku baadhi ya raia wakiamua kuelekea kwenye shuhuli zao kwa mguu.
Kaskazini kama magharibi mwa jiji la Bujumbura nimeshuhudia hatua hiyo ya waziri wa mambo ya ndani, maendeleo ya jamii na usalama Gervais Ndirakoca, ya kupiga marufu bodaboda, Pikipiki na baskeli kuingia mjini kati imeheshimishwa.
Baadhi ya raia nimeshuhudia wakibeba mizigo kichwani, na kutembea kwa mguu. Huku wengine walosubiri mabasi katika mitaa ya kaskazini mwa jiji wamelalamika ya kuwa kupigwa marufu bodaboda, Pikipiki na baskeli kumewasababishia usumbufu mkubwa.
"Nilikuwa nikitumia piki piki ama baskeli ili niweze kufika kwenye, eneo langu la shuhuli, lakini sasa naona raia tutaabika kweli. Itakuwa vigumu kufika kazini kwa wakati unaofaa. Hii ni hatari kwa kweli," amesema abiria mmoja ambaye hutumia bodaboda.
Mtumiaji mwengine pia ameelezea wasiwasi wake akisema "hali inaelekea kuwa ngumu, mimi nilikuwa nikitumia usafiri wa piki piki nanunuwa daga kwenye soko ya cotebu na kwenda kuziuza mtaani Gasenyi. Sina uwezo mkubwa wa kukodi gari hivyo kazi yangu naona imeharibika."
Raia huyu hapa mwengine anasema kinyume na kawaida hata basi imekuwa vigumu leo kupatikana, kufuatia uhaba wa mafuta ya gari uliopo nchini. Mabasi yaloweza kufanya kazi yalionekana kuishia mbali na vituo vya kupakiria abiria mitaani.
Hatua hii ya kupigwa marufuku bodaboda piki piki na baskeli kufika jijini kati imetekelezwa baada ya kumalizika muda wa ziada wa siku 10 ulongezwa na waziri Ndirakobuca aloagiza kuoroddheshwa wote walokuwa wakiendesha vifaa hivyo.
Tangu usiku wa manene polisi ya taifa ilipiga doria kwenye maeneo ambako kulikuwa na ishara ya kuvikataza vifaa hivyo vya usafiri kutozidi, wakati kulikuwepo na uvumi wa kufanyika maandamano ili kupinga hatua hiyo.
Mapema alfajir milio ya risasi ilisikika, na taarifa zinasema kuwepo na watu wawili walopoteza maisha baada ya kutaka kukiuka sheria hiyo. Hata hivyo Polisi ya taifa haikuthibitisha taarifa hiyo.