1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAF yamuunga mkono Sheikh Salman

6 Februari 2016

Ndoto ya Sheikh Salman kumrithi Sepp Blatter imepigwa jeki wakati Shirikisho la kandanda Afrika – CAF kutangaza kuwa linamuunga mkono afisa huyo wa Bahrain kuwa rais wa Shirikisho la Kandanda Duniani – FIFA

https://p.dw.com/p/1Hqn8
Bahrain FIFA Sheikh Salman bin Ebrahim Al Khalifa
Picha: picture-alliance/AP Photo/H. Jamali

Kufuatia mkutano wa viongozi wa kandanda Afrika uliofanyika mjini Kigali Rwanda hapo jana, Kamati Kuu ya CAF ilitangaza kuwa itamuunga mkono kikamilifu rais huyo wa shirikisho la kandanda la Asia. SUKETU Patel ni makamu rais wa CAF

Salman na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kandanda Ulaya – UEFA Gianni Infantino wanaonekana kuwa wagombea wakuu wanaotarajiwa kushinda uchaguzi huo wa Februari 26. Bara la Afrika ndilo lenye kura nyigni zaidi katika uchaguzi wa rais wa FIFA likiwa na 54.

Salman na Infantino wanatarajiwa kupata uungwaji mkono kutoka kwa mabara yao, Asia na Ulaya. Lakini Afrika inaonekana kuwa ni bara litakalohakikisha ushindi kwa mmoja wao. Kwa kumuunga mkono Salman, CAF pia ilimpiga kumbo mgombea pekee wa Afrika katika orodha hiyo ya wagombea watano, mfanyabiashara wa Afrika Kusini Tokyo Sexwale.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Josephat Charo