CARACAS: Hugo Chavez ajiondoa kutoka kwa taasisi za kimataifa
1 Mei 2007Matangazo
Rais wa Venezuela Hugo Chavez alitangaza jana kwamba nchi yake itajiondoa kutoka kwa benki ya dunia na shirika la fedha la kimataifa, IMF.
Rais Chavez anazishutumu taasisi hizo kwa kuzinyanyasa nchi ndogo. Aidha amesema taasisi hizo ni vyombo vinavyotumiwa na Marekani kuendeleza ubabe wake.
Rais Chavez amesema nchi yake itajiondoa kutoka kwa taasisi hizo na kudai kila kitu kilichokuliwa na taasisi hizo, akidai kwa sasa zimo katika matatizo makubwa kifedha huku zikiwa hazina fedha za kutosha kulipa mishahara ya wafanyakazi wake.