CARACAS:Chavez atangaza kutaifisha makampuni makubwa nchini Venezuela
9 Januari 2007Matangazo
Rais Hugo Chavez wa Venezuela ametangaza mipango ya kubinafsisha kampuni za umeme na simu nchini humo ikiwa ni katika hatua kuelekea katika taifa la kisoshalisti.
Chavez akihamasishwa na siasa za kiongozi wa Cuba Fidel Castro amesema kuwa , hatua hiyo ni katika kuelekea kuunda jamuhuri ya kisoshalisti ya Venezuela.
Kiongozi huyo anatarajiwa kuapishwa kesho kwa kipindi cha tatu cha Urais kufuatia ushindi wake mkubwa katika uchaguzi mkuu wa mwezi uliyopita.