CCM: maoni ya walalamikaji kuhusu DP World si ya kupuuzwa.
2 Agosti 2023Duru zinaelezakuwa chama hicho kipo tayari kuishauri serikali kuupitia mkataba huo ili kuboresha maeneo yanayotajwa kuwa na mapungufu.
Hatua hiyo ni tofauti na msisitizo wake iliouweka awali kwamba inaunga mkono mkataba huo kwa madai kwamba ulikuwa imezingatia maslahi yote ya taifa.
Hivi sasa viongozi wa chama cha CCM ambao wanazunguka katika maeno mbalimbali ya nchi kuendesha mikutano ya wazi, wanakiri kuwepo kwa mapungufu kwenye mkataba huo kwa vile walioupitisha ni binadamu.
CCM: Serikali haipaswi kuyapuuza malamiko ya mkataba wa bandari.
Katibu mkuu wa chama hicho anayeambatana na makada katika mikutano hiyo, Daniel Chongolo amesema serikali haipaswi kuendelea kuyapa kisoga malalamiko yanayotolewa na wananchi na kwamba serikali hiyo inapaswa kuutazama mkataba huo na kuridhia marekebisho.
Hatua hiyo ya chama tawala inakuja wakati sakata kuhusu mkataba huo likiendelea kuwa mada moto huku chama kikuu cha upinzani Chadema kikiendelea kuwasambaza viongozi wake wanaozunguka kila kona ya nchi kuupinga mkataba huo uliosainiwa baina ya serikali na kampuni ya kigeni ya DP World ya Dubai.
Wakosaji: Makataba wa kampuni ya kigeni ya DP World ya Dubai haujazingatia maslahi ya taifa.
Baadhi ya wale wanaoukusoa wanasema mkataba huo, haujazingatia maslahi ya taifa huku ukitoa upendeleo mkubwa kwa mwekezaji huyo wa kigeni.
Katika hatua nyingine, mwanaharakati na mwanasheria anayeupinga mkataba huo, Boniface Mwabukusi amesema hatorudi nyuma katika kampeni yake ya kuupinga mkataba huo licha ya kile alichokisemwa kuandamwa huku na kule.
Wakili huyo wa kijitegemea anasema amepokea barua kutoka kwa kamati ya maadili inayosimamia mawakili nchini, inayomtaka kujieleza kutokana na tuhumu za uvunjifu maadili zinazomkabili.
Sma zaidi:Upinzani wanusa harufu ya ufisadi Zanzibar
Licha ya kuwepo kwa baadhi ya watendaji wa serikali wanaojitokeza hadharani kuutetea mkataba huo, hadi sasa serikali bado haijatoa msimamo wake wa mwisho kuhusu sakata hilo hali ambayo imezidisha malumbano kwa makundi ya waoutetea na wale wanaoukosoa.
DW: Dar es Salaam