1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chad yadai kuwaua wanamgambo wengi wa Boko Haram

8 Novemba 2024

Rais wa Chad Mahmat Idriss Deby Itno amesema wapiganaji wengi wameuwawa na kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya jeshi la nchi hiyo yaliyowalenga wanamgambo wa kundi la itikadi kali za Kiislamu la Boko Haram.

https://p.dw.com/p/4mmyX
Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby Itno
Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby ItnoPicha: MOUTA/dpa/picture alliance

Rais wa Chad Mahmat Idriss Deby Itno amesema wapiganaji wengi wameuwawa na kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya jeshi la nchi hiyo yaliyowalenga wanamgambo wa kundi la itikadi kali za Kiislamu la Boko Haram.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Alhamisi, Deby amesema alielekeza mashambulizi kwa wanamgambo hao ambao walilishambulia jeshi la Chad mwezi uliopita katika eneo la magharibi karibu na mpaka wa Nigeria na kuwauwa takriban watu 40 na kuwajeruhi watu wengine kadhaa.

Soma: Mahamat Itno aapishwa kuwa rais wa Chad

Wiki iliyopita,  Waziri Mkuu wa mpito Abderahim Bireme Hamid  alitamka kuwa, operesheni ya jeshi la Chad dhidi ya wanamgambo hao inalenga si tu kuhakikisha amani kwa raia bali pia kuwakamata na kuharibu uwezo wa Boko Haram na washirika wake wa kusababisha madhara.