SiasaAfrika Kusini
Chama cha MK chajaribu kuzuia vikao vya kwanza vya bunge
11 Juni 2024Matangazo
Bunge jipya la Afrika Kusini lililochaguliwa katika uchaguzi wa mwezi uliopita, linatarajiwa kukutana siku ya Ijumaa kuwaapisha wabunge wapya. Pia litamchagua spika na naibu wake pamoja na rais wa taifa hilo.
Chama cha MK kwa mshangao kiliibuka nafasi ya tatu katika uchaguzi wa Mei 29. Chama hicho kimedai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu na kimetishia kususia bunge jipya.
Tume huru ya uchaguzi na vyama vingine vinadai kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na haki na kwamba Afrika Kusini haina historia ya udanganyifu katika chaguzi.
Chama tawala cha ANC kilipoteza wingi wa kura bungeni kwa mara ya kwanza tangu kilipoingia madarakani miaka 30 iliyopita.