SiasaAfrika Kusini
Chama cha Zuma cha pinga kikao cha bunge cha kumchagua rais
12 Juni 2024Matangazo
Chama cha Zuma cha uMkhonto weSizwe kimesema wabunge 58 wapya wa chama chake hawatohudhuria kikao hicho.
Chama hicho cha MK, kinaitaka Mahakama ya Katiba kutouzingatia uamuzi wa Tume ya Uchaguzi nchini humo kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki.
Kinataka rais aamrishwe kuitisha uchaguzi upya. Chama hicho cha Zuma kilikuwa kimewasilisha pingamizi kwa Tume ya Uchaguzi kikidai kulikuwa na wizi wa kura katika uchaguzi wa kitaifa wa mwezi uliopita. uMkhonto weSizwe kilipata asilimia 14 tu ya kura zilizopigwa.