1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Chama tawala Korea Kaskazini chagawika kuhusu rais

5 Desemba 2024

Mnadhimu mkuu wa chama tawala nchini Korea Kusini ameapa kwamba wabunge wote wa chama hicho wataungana kupinga kuondolewa madarakani Rais Yoon Suk Yeol kufuatia kiongozi huyo kutangaza sheria ya kijeshi nchini humo.

https://p.dw.com/p/4nlIf
Seoul 2024 | Yoon Suk Yeol
Wapinzani wakiandamana dhidi ya Rais Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini.Picha: Ahn Young-joon/AP Photo/picture alliance

Choo Kyung-ho amesema wabunge wote 108 wa Chama cha Nguvu za Umma wataungana kukataa hoja hiyo. Upinzani unahitaji angalau wabunge wanane wa chama tawala kupitisha hoja yao.

Soma zaidi: Upinzani Korea Kusini wawasilisha mswada wa kumuondoa rais Yoon

Kauli ya mnadhimu huyo wa chama tawala inakuja wakati tayari mkuu chama hicho, Han Dong-hoon, akiwaambia waandishi wa habari kwamba amemtaka Rais Yoon aondoke kwenye chama hicho na kwamba chama chake hakitajaribu kumlinda rais huyo na sheria yake inayokwenda kinyume na katiba.

Tayari waziri wa ulinzi, Kim Yong-hyun, amejiuzulu na nafasi yake kuchukuliwa na balozi wa Korea Kusini nchini Saudi Arabia, Choi Byung-hyuk.