Angela Merkel ameanza muhula wake wa nne madarakani kama kansela wa Ujerumani, baada ya miezi sita ya mashaka. Anakabiliwa na vishindo, ikiwa ni pamoja na kuibuka makundi ya siasa kali za kizalendo nchini Ujerumani, kuwakilishwa kwa mara ya kwanza katika bunge chama cha siasa kali za mrengo wa kulia Chaguo Mbadala kwa Ujerumani, AfD, na miito ya kufanyiwa marekebisho Umoja wa ulaya.