Utayarishaji wa filamu zinazowakosoa watawala au jamii kwa ujumla hukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo nyingine huwakwamisha wasanii wenye vipaji na kuwanyima fursa ya kujiendeleza katika taaluma zao.
Inahitaji wasanii mahiri wenye ukakamavu na shujaa kuweza kuandaa filamu zenye ujumbe mzito unaokusudiwa bila kuogopa matokeo yanayoweza kutokea. Katika Kinagaubaga Josephat Charo amezungumza na Amil Shivji, mtayarishaji wa filamu kutoka Tanzania.