SiasaChina
China kuimarisha uhusiano wake na Korea Kaskazini
12 Septemba 2023Matangazo
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Mao Ning ameuambia mkutano wa waandishi habari kuwa uhusiano wa China na Korea Kaskazini unaendelea vizuri.
Shirika la habari la serikali la Urusi Ria Novosti limeripoti kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amewasili nchini humo leo.
Soma pia:Biden azungumza na Waziri mkuu wa China
Kulingana na msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov, kiongozi huyo wa Korea Kaskazini anatarajiwa kukutana na Rais Vladimir Putin baadaye wiki hii.
Ziara hiyo ni kwanza kwa Kim kuifanya nje ya nchi tangu janga la UVIKO-19.