China kushiriki mazungumzo kuhusu mpango wa amani wa Ukraine
5 Agosti 2023Mazungumzo hayo yaliyoitishwa na Saudia, yanatarajiwa kufanyika mjini Jeddah kuanzia leo na kuwakutanisha wanadiploamsia wa Ukraine, nchi za Magharibi, washauri wa kitaifa wa usalama na maafisa waandamizi kutoka nchi takribani 40.
Soma zaidi: China yatoa wito wa kuanzishwa tena usafirishaji wa nafaka
Wajumbe katika mazungumzo hayo ya siku mbili watakubaliana juu ya mpango wa amani wa kumaliza vita ya Urusi nchini Ukraine. Rais Volodmyr Zelensky amesema mapema wiki hii kwamba ana matumaini mpango huo utafungua njia kuelekea mkutano wa kilele wa amani wa viongozi wa ulimwengu baadae mwaka huu ili kujadili vipengele vya utatuzi wa mzozo na Jirani yake.
Urusi haikualikwa katika mazungumzo ya mjini Jeddah. Saudi Arabia imejitolea mara kwa mara kupatanisha Urusi na Ukraine.