1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China na Marekani wakubaliana kuandaa mkutano wa Xi na Biden

28 Oktoba 2023

China na Marekani wamekubaliana kushirikiana kuandaa mkutano kati ya rais Xi Jinping na Joe Biden, afisa mwandamizi wa serikali ya Biden amesema Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4Y8Xg
Mawaziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi na Anthony Blinken (kulia) wa Marekani walipokutana kwa mazungumzo mjini Washington, Oktoba 26,2023
Mawaziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi na Anthony Blinken(kulia) wa Marekani walipokutana kwa mazungumzo mjini Washington, Oktoba 26,2023Picha: Saul Loeb/AFP/Getty Images

Maafisa hao hata hivyo walipozungumza na waandishi wa habari hawakufafanua zaidi ikiwa mkutano huo utafanyika pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Ushirikiano wa kiuchumi kwa Mataifa ya Asia na Pasifiki, APEC mwezi ujao huko San Francisco.

Matamshi haya yanatolewa baada y mazungumzo yaliyodumu kwa masaa kadhaa kati ya waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi na maafisa hao mjini Washington.

Wang Yi, waziri wa kwanza wa mambo ya nje wa China kuzuru Marekani tangu mwaka 2018, alikutana kwanza na rais Biden, waziri wa mambo ya nje Anthony Blinken pamoja na mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa White House, Jake Sullivan.