1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China na Marekani zaahidi ushirikiano wa mambo ya mazingira

15 Novemba 2023

Rais wa kongamano la 28 la Umoja wa Mataifa la mazingira Sultan Al Jaber amesema kuwa tamko la pamoja la Marekani na China kuhusu tabianchi ni hatua muhimu kuelekea mkutano huo wa kimataifa.

https://p.dw.com/p/4YqbG
Mkutano wa Mazingira Bonn | Sultan Ahmed Al Jaber
Rais wa kongamano la 28 la Umoja wa Mataifa la mazingira Sultan Ahmed Al JaberPicha: Sascha Schuermann/Getty Images

Lakini baadhi ya watalaamu wamekosoa ukosefu wa ahadi thabiti katika tamko hilo. Sultan Al Jaber amesema katika taarifa, tamko hilo linaashiria wazi kuwa licha ya changamoto za ulimwengu, wito wa mkutano wa COP28 wa kuchukuliwa hatua ya tabianchi unawaunganisha wahusika na kuongeza dhamira.

China na Marekani zimeahidi leo kushirikiana kwa karibu zaidi katika kupambana na ongezeko la joto ulimwenguni.

Maandalizi ya COP28 yaanza Bonn

Zimetangaza kuwa mgogoro wa tabianchi ni mojawapo ya changamoto kubwa kabisa za nyakati zetu.

Tangazo hilo limejiri saa chache kabla ya mkutano wa kwanza kufanyika katika mwaka mmoja kati ya Marais Joe Biden na Xi Jinping, pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia-Pasifik mjini San Francisco.