SiasaAsia
China, Urusi zafanya doria pamoja Bahari ya Pasifiki
14 Julai 2024Matangazo
Kulingana na taarifa iliyotolewa Jumapili 14.07.2024 na televisheni ya taifa ya China CCTV, zoezi hilo ni sehemu ya mpango wa pamoja wa kila mwaka kati ya mataifa hayo hayo mawili.
Soma zaidi: Urusi na China zafanya luteka za pamoja za kijeshi
Taarifa hiyo hata hivyo imebainisha kuwa, mpango huo hauilengi nchi nyingine yoyote. Imeongeza pia kuwa, hatua iliyochukuliwa na China na Urusi, haihusiani kwa namna yoyote na hali ya sasa ya kimataifa na kikanda. Hii ni mara ya nne kwa nchi hizo mbili kufanya doria ya pamoja katika eneo hilo la bahari.
China na Urusi zimeimarisha mahusiano yao ya kiuchumi na kijeshi, jambo linalozusha hofu na mashaka kwa mataifa ya Magharibi ambayo yanalenga kukabiliana na ushawishi unaoongezeka wa China.