1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yaelezea madai ya Ujerumani kuwa ya kizushi

26 Aprili 2024

Msemaji wa wizara ya mbao ya nje ya China wang Webin amesema Ijumaa kwamba madai ya kukamatwa kwa Wajerumani wanne wanaotuhumiwa kuifanyia China ujasusi ni ya uwongo.

https://p.dw.com/p/4fDKc
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Wang Wenbin
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Wang WenbinPicha: Mark Schiefelbein/AP

China imesema kuwa madai ya kukamatwa kwa Wajerumani wanne wanaotuhumiwa kuifanyia China ujasusi nchini Ujerumani ni ya uwongo. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema tuhuma zinazotolewa ni za kizushi.

 "Kesi ya watu kuifanyia ujasusi China ni ya uwongo. Shutuma za Ujerumani hazina msingi wowote. Tunataka kusema kwa mara nyengine tena kwamba China inapinga hatua zotzote za kuiharibia jina na kuipaka tope na tunaiomba Ujerumani kutoharibu mahusiano ya mataifa haya mawili. Tunaitaka kujizuwia kufanya hivyo na kulinda kwa dhati uthabiti na maendeleo mazuri ya mahusiano yetu.", Wenbin alisema.

Jana Alhamisi Balozi wa Ujerumani nchini China alisema aliitwa na utawala wa Beijing kuelezea tukio hilo. Watu hao waliokamatwa magharibi mwa Ujerumani siku ya Jumatatu wanakabiliwa na madai ya kutoa taarifa ya teknolojia ya baharini kwa China.

Baadae siku ya Jumanne msaidizi wa mbunge wa bunge la Ulaya kutoka Ujerumani Maximilian Krah wa chama cha AFD alikamatwa kwa madai ya kutoa taarifa za bunge hilo kwa China na kuwachunguza wapinzani wa China nchini Ujerumani.

China imeionya Ujerumani kuwa makini isije ikatia doa mahusiano ya mataifa hayo mawili.