China yaifuta ziara ya Mkuu wa Sera za Kigeni wa EU
5 Julai 2023Umoja wa Ulaya umesema kuwa China imeifuta ziara ya mwanadiplomasia mkuu wa umoja huo Josep Borelliliyopangwa kuanza Julai 10 katika wakati pande hizo mbili zinatofautiana pakubwa juu ya masuala muhimu ikiwemo biashara, haki za biandamu na vita nchini Ukraine.
Msemaji wa umoja huo Nabila Massarali amesema wamearifiwa na wenzao wa China kuwa ziara ya mkuu ya sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya mjini Beijing haitaweza kufanyika kwa tarehe zilizoainishwa hapo kabla bila ya kutoa sababu.
Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wakutana Luxemburg
Wakati wa ziara hiyo Borell alikuwa amepangiwa kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nchi za nje wa China Qin Gang na wanadiplomasaia wengine wa nchi hiyo kuhusu biashara, haki za binadamu na msimamo wa Beijing kuhusu vita vya Ukraine.
Kwa upande wake China imesema inathamini mahusiano kati yake na Umoja wa Ulaya na itatafuta muda mwafaka wa kumaribisha tena Borell kuitembelea nchi hiyo.