China yaimarisha ulinzi dhidi ya janga la virusi vya Corona
26 Januari 2020
Wakati huo huo Marekani, Ufaransa na Japan zinajitayarisha kuwaondoa raia wao kutoka katika mji ulioko katika karantini ambao ndio chimbuko la virusi hivyo wa Wuhan.
China imezuwia watu kuingia ama kutoka kutoka katika mji ulioathirika zaidi katika jimbo la Hubei katikati ya nchi hiyo katika operesheni kamambe inayowaathiri mamia kwa mamilioni ya watu ili kuweza kupunguza kasi ya ugonjwa huo unaoathiri njia ya kupumua.
Uwezo wa virusi hivyo kusambaa "unaonekana kuwa imara zaidi , licha ya kuwa , si vyenye nguvu sana kama virusi vya SARS", maafisa wa afya wa ngazi ya juu nchini China wamesema katika mkutano na waandishi habari, na kuongeza kuwa uelewa wao kuhusu virusi hivyo una mipaka.
Virusi vya hapo kabla visivyojulikana vilisababisha wasi wasi mkubwa duniani kwasababu ya ukaribu wake kama virusi vya SARS, virusi vilivyosababisha matatizo makubwa ya kupumua, ambavyo vimeuwa mamia ya watu nchini China na Hong Kong mwaka 2002-2003.
Nje ya eneo ulipoanzia ugonjwa huo, miji minne, ikiwa ni pamoja beijing na Shanghai, na jimbo la mashariki la Shandong, imetangaza marufuku kwa mabasi yanayosafirisha abiria masafa marefu kuingia ama kutoka katika mipaka yake, hatua ambayo itawaathiri mamilioni ya watu wanaosafiri kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya.
Wakaazi kuvaa vizuwizi usoni
Jimbo maarufu la mashariki la Guandong, Jiangxi katikati ya nchi hiyo, na miji mitatu imeweka ulazima kwa wakaazi kuvaa vifunika uso wakiwa katika maeneo ya watu wengi.
Ukianzia katika mji mkuu wa jimbo la Wuhan , Hubei, virusi hivyo vilisambaa nchini China na duniani , ambapo maambukizi yalithibitishwa katika karibu nchi 12 hadi Marekani.
Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani imesema leo Jumapili (26.01.2020) kuwa inapanga safari ya ndege kutoka Wuhan kwenda San Francisco kwa wafanyakazi wake wa ubalozi mdogo pamoja na Wamarekani wengine katika mji huo.
Safari hiyo ya ndege siku ya Jumanne, imesema katika taarifa ya barua pepe kwa Wamarekani wote nchini China ambayo inaonya, uwezo mdogo sana kwa kuwachukua raia wa kawaida.
Serikali ya Ufaransa na kampuni ya Ufaransa ya kuunda magari ya PSA pia imesema wanatayarisha mipango kuwaondoa wafanyakazi na famiali zao , ambao wanawekwa katika karantini katika mji uliopo katika jimbo jirani.
Japan inafanya uratibu na serikali ya China kuwaondoa haraka raia wake, waziri mkuu Shinzo Abe amesema.
Ubalozi mdogo wa Korea kusini mjini Wuhan umesema unafanya taratibu za kuwahesabu raia wake kupitia mtandaoni ili kujua mahitaji ya ndege za kukodi zinazohitajika.