1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yajitolea kuwa mpatanishi wa Iran na Pakistan

18 Januari 2024

China imesema kwamba iko tayari kuwa mpatanishi kati ya Pakistan na Iran kufuatia mashambulizi dhidi ya wanamgambo katika eneo la mpakani, ikiwemo shambulizi ambalo Iran inasema limewauwa raia saba.

https://p.dw.com/p/4bPfn
China /Mao Ning
Waziri wa masuala ya nchi za nje wa China Mao Ning Picha: Andy Wong/AP Photo/picture alliance

Iran imemuamrisha balozi wake nchini Pakistan kurudi nyumbani kufuatia shambulizi hilo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning amewaambia waandishi wa habari kwamba China inatumai kuwa pande hizo mbili zinazozozana zitadumisha utulivu na kuzuia kuongezeka kwa mivutano.

Mzozo mpya waibuka kati ya Pakistan na Iran

Mashambulizi hayo yanayaweka mashakani mahusiano ya kidplomasia kati ya nchi hizo majirani kwani kwa muda mrefu, Iran na Pakistan iliyojihami kwa silaha za nyuklia, zimekuwa na shauku kuhusiana na mashambulizi ya wanamgambo.