1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yamuonya Spika wa Marekani kuhusu Rais wa Taiwan

4 Aprili 2023

China imemuonya spika wa baraza la wawakili la Marekani Kevin McCarthy asirudie makosa ya zamani yaliyosababisha majanga na kukutana na rais wa Taiwan Tsai Ing-wen.

https://p.dw.com/p/4PfmN
Guatemala | Taiwans Präsidentin Tsai Ing-wen beim Besuch von Tikal
Picha: Moises Castillo/AP/picture alliance

McCarthy atakutana na Tsai kesho Jumatano mjini Los Angeles jimboni Carlifornia wakati atakapopitia Marekani akiwa njiani kurejea nyumbani Taiwan baada ya ziara yake ya Amerika ya Kaskazini.

Soma pia: Rais wa Taiwan awasili Amerika ya Kati akitafuta ushirika zaidi

China imeghadhabishwa na hatua hiyo na imetahadharisha kwamba mkutano kati ya McCarthy na Tsai hautasaidia amani na uthabiti wa kikanda bali utawaunganisha umma wa China dhidi ya adui mmoja.

Ubalozi mdogo wa China mjini Los Angeles umesema Tsai anafanya mazungunzo rasmi na sio sahihi kusema anapitia tu Marekani.

Ubalozi huo umeongeza kusema mkutano kati ya McCarthy na Tsai haufai kwa amani, usalama na uthabiti wa kikanda na wala si wa masilahi ya watu wa China wala Marekani.