1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yaonya dhidi ya uingiliaji wa kigeni suala la Taiwan

14 Aprili 2023

China imepinga vikali uingiliaji wowote wa kigeni juu ya suala la hadhi ya kisiwa cha Taiwan na kuyahimiza mataifa mengine kuheshimu msingi unaotambulika kimataifa wa "China moja".

https://p.dw.com/p/4Q5NA
Waziri Mkuu wa mambo ya nje wa China Qin Gang
China inadai kuwa kisiwa kinachojitawala cha Taiwan ni sehemu ya himaya yakePicha: Suo Takekuma/Pool via REUTERS

China leo imepinga vikali uingiliaji wowote wa kigeni juu ya suala la hadhi ya kisiwa cha Taiwan na kuyahimiza mataifa mengine kuheshimu msingi unaotambulika kimataifa wa "China moja".

Soma pia: Baerbock aionya Ulaya kuhusu kuufumbia macho mvutano kati ya China na Taiwan

Waziri wa mambo ya kigeni wa China Qin Gang amewaambia waandishi habari mjini Beijing kuwa Taiwan ni sehemu ya China na taifa hilo halitaruhusu nguvu kutoka nje kubadili ukweli huo. Gang alikuwa akizungumza baada ya kukutana na waziri wa mambo ya nje za nje wa Ujerumani Annalena Baerbock anayeitembelea China tangu jana Alhamisi.

Soma pia: China yahitimisha luteka za kijeshi kuizunguka Taiwan

Akiwa nchini humo Bibi Baerbock amesisitiza kwamba Ujerumani inazingatia "Sera ya China moja" lakini hakusita kugusia mvutano unaendelea sasa kwenye ujia wa bahari wa Taiwan na kuhimiza umuhimu wa kutulizwa mzozo uliopo kwa njia ya amani.