China yapiga marufuku uingizwaji bidhaa za bahari za Japan
24 Agosti 2023Matangazo
Japan ilianza kuyatiririsha maji hayo yaliyosafishwa na kuondolewa viambata vya mionzi kutoka kinu hicho cha nyuklia cha Fukushima kilichoharibiwa na tetemeko kubwa la ardhi na kuelekea kwenye Bahari ya Pasifiki, katika operesheni ambayo inasisitiza ni salama.
Wizara ya mambo ya nje ya China imeitaja hatua hiyo kama ni ya "kibinafsi na ya kutowajibika" na kusema inaweza ikachochea hatari ya usalama wa chakula kote ulimwenguni kutokana na uchafuzi wa mionzi kwenye chakula.