1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yatia saini mikataba kadhaa na Chad na Senegal

Sylvia Mwehozi
5 Septemba 2024

China imetia saini mikataba kadhaa na Chad na Senegal inayohusisha miradi ya umeme, miundombinu na teknolojia ya mawasiliano. Mikataba hiyo imesainiwa kwenye mkutano wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika.

https://p.dw.com/p/4kHwD
China Peking | China-Afrika-Kooperationsforum
Bendera za mataifa ya afrika yanayoshiriki Kongamano la China-AfrikaPicha: ADEK BERRY/AFP

China imetia saini mikataba kadhaa na Chad na Senegal inayohusisha miradi ya umeme, miundombinu na teknolojia ya mawasiliano. Mikataba hiyo imesainiwa pembezoni mwa mkutano wa kilele wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrikamjini Beijing. China ambayo ni mkopeshaji mkubwa zaidi wa nchi hizo mbili, imeyaalika mataifa 50 ya Afrika ikilenga kurekebisha uhusiano wake na nchi zinazoendelea kiuchumi.

Miradi ya Chad itahusisha uboreshaji wa miundombinu ya umeme na maji salama ya kunywa katika mji mkuu wa N'Djamena na ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa ndege nje ya mji huo. Katika taarifa tofauti, Ofisi ya rais wa Senegal ilisema kuwa nchi hiyo imetia saini takriban mikataba kumi na mbili na China, ikiwa ni pamoja na teknolojia ya habari na mawasiliano, maendeleo ya mazingira na vyombo vya habari.