1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yazungumza na Myanmar kuhusu usalama wa mipaka

31 Oktoba 2023

Waziri wa usalama wa umma wa China amefanya mazungumzo na watawala wa kijeshi wa Myanmar kuhusu ulinzi na usalama kwenye mpaka wao wa pamoja.

https://p.dw.com/p/4YDzE
Myanmar | Kachin-Staat Soldaten
Makundi ya wapiganaji yanakabiliana na wanajeshi wa Myanmar mpakani mwa nchi hiyo na China.Picha: Esther Htusan/AP Photo/picture alliance

Hii inatokana na makabiliano kati ya makundi ya wapiganaji na jeshi nchini Myanmar.

Wang Xiaohong, ambaye pia ni mjumbe wa baraza la mawaziri la China linalofahamika kama Baraza la Taifa, alikutana na waziri wa mambo ya ndani wa utawala wa kijeshi wa Myanmar, Luteni Jenerali Yar Pyae, katika mji mkuu wa Myanmar, Naypyidaw.

Soma zaidi: Kambi ya wakimbizi Myanmar yashambuliwa kwa kombora

Maelfu ya watu wameripotiwa kuyahama makaazi yao, huku baadhi wakiingia China, baada ya makundi matatu yenye silaha yanayopigania uhuru kuanzisha mashambulizi yaliyoratibiwa dhidi ya utawala wa kijeshi, ambao ulisema umepoteza udhibiti wa vituo kadhaa.

Makundi hayo matatu -- ambayo wachambuzi wanasema yanaweza kuwakusanya wapiganaji 15,000 kati yao, yamepigana mara kwa mara na jeshi kudai uhuru na udhibiti wa raslimali.