COLOGNE: Chama cha Kijani Ujerumani kitachunguza tume za kijeshi
4 Desemba 2006Matangazo
Chama cha upinzani cha Kijani nchini Ujerumani kimejadiliana juu ya dhima ya Ujerumani nchini Afghanistan,huku ikitolewa miito ya kubadilisha mkakati wa kijeshi.Baadhi ya wanachama wa mrengo wa shoto katika chama cha Kijani kwenye mkutano wao mjini Cologne,wamesema wanajeshi wa Kijerumani walio sehemu ya vikosi vya amani vya kimataifa nchini Afghanistan,waondoshwe kutoka eneo hilo la mgogoro.Viongozi wa chama hicho lakini wameipinga fikra hiyo wakiwa na hofu kuwa uamuzi wa aina hiyo huenda ukaeleweka visisvyo katika nchi za ngámbo.Kwa hivyo badala yake, wajumbe mkutanoni walipiga kura kuunda halmshauri itakyochunguza tume za kijeshi za Ujerumani,chini ya uongozi wa waziri wa kigeni wa zamani Joschka Fischer.