1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOGNE: Jung kuvitembelea vikosi vya Kijerumani

24 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD9K

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung hii leo ameanza ziara yake ya siku tatu barani Afrika.Kituo chake cha kwanza ni Djibouti ambako kikosi cha wanamaji wa Kijerumani kinashiriki katika operesheni ya kupiga vita ugaidi duniani.Takriban wanajeshi 350 wa Kijerumani wanasaidia kupiga doria katika mwambao wa Pembe ya Afrika.Baada ya Djibouti,waziri Jung atakwenda Gabon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Wanajeshi wa Kijerumani walipelekwa Kongo kulinda usalama wakati wa uchaguzi wa rais uliofanywa mwezi wa Julai.Duru ya pili imepangwa kufanywa mwezi Okotoba.Waziri Jung anatazamia kukutana na Rais Joseph Kabila na pia kiongozi wa upinzani, Jean-Pierre Bemba mjini Kinshasa.