1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOGNE : Merkel ataka Afrika isidharauliwe

10 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtD

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa Kanisa la Kiprotestanti mjini Cologne amesisitiza umuhimu wa kutimizwa kwa viwango vya kijamii na mazingira duniani kwa ajili ya ulinzi wa raia.

Kansela Merkel amesema viwango vya kijamii na mazingira vinahitajika duniani kote na kwamba hiyo ni njia pekee ya kufanikiwa kwa utandawazi na kuwa viwango hivyo havipaswi kushushwa kwa mujibu tu mtu anavyotaka.

Katika kuulezea Mkutano wa Kundi la Mataifa Manane yenye maendeleo makubwa ya viwanda duniani amesema maamuzi yaliofikiwa ni makubwa sana licha ya kwamba mkutano huo baadae ulikosolewa vikali.

Kiongozi huyo wa Ujerumani amesisitiza kwamba Ulaya haiwezi kujikweza wakati inaposhughulikia suala la Afrika.

Katika mkutano wa G8 viongozi wa mataifa hayo tajiri kabisa duniani wameahidi kutowa euro bilioni 44 kupiga vita UKIMWI malaria na kifua kikuu barani Afrika na kutekeleza ahadi za misaada ya fedha.