1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOGNE: Vikosi vya mwanzo vya Ujerumani vimeondoka Kongo

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCn4

Vikosi vya mwanzo vya Kijerumani,vilivyokuwa sehemu ya majeshi ya Umoja wa nchi za Ulaya-EUFOR-vimerejea nyumbani,baada ya kukamilisha ujumbe wake nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Kama wanajeshi 100 kutoka jumla ya 780 walitua asubuhi ya leo kwenye uwanja wa ndege wa Cologne-Bonn.Baada ya ujumbe wa vikosi hivyo vya EUFOR kumalizika siku ya Alkhamisi,wanajeshi wote 780 wa Ujerumani wanatazamiwa kurejea nyumbani hadi ifikapo Desemba 23.Vikosi hivyo vilikuwa na ujumbe wa kusimamia usalama wakati wa kufanywa uchaguzi huru wa mwanzo baada ya takriban miongo minne,nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.