COLOGNE: Wanajeshi zaidi wapelekwa Kongo
16 Julai 2006Matangazo
Kundi jingine la wanajeshi wa Kijerumani wapatao 170 limeondoka Cologne leo hii kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Kundi hilo litaungana na wanajeshi wa Kijerumani waliotangulia.Wanajeshi 780 wa Kijerumani watasaidia kulinda usalama wakati wa kufanywa uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Uchaguzi huo umepangwa kufanywa tarehe 30 mwezi huu wa Julai.Pamoja na Ufaransa,Ujerumani imebeba dhamana kuu ya kikosi cha walinzi wa amani wapatao 2,000 kutoka nchi za Umoja wa Ulaya,wengi wao wakiwa katika mji mkuu Kinshasa.