1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cologne yamwonyesha mlango kocha Solbakken

13 Aprili 2012

Klabu ya FC Cologne imempiga kalamu kocha Stale Solbakken ikiwa imesalia mechi nne msimu wa ligi kuu ya soka Ujerumani - Bundesliga ukikamilika. Kocha wa zamani Frank Schaefer amerejea tena katika wadhifa huo.

https://p.dw.com/p/14dmc
FC Cologne coach Stale Solbakken reacts during their German first division Bundesliga soccer match against FSV Mainz 05 in Mainz April 10, 2012. REUTERS/Kai Pfaffenbach (GERMANY - Tags: SPORT SOCCER) DFL LIMITS USE OF IMAGES ON THE INTERNET TO 15 PICTURES DURING THE MATCH AND, PROHIBITS MOBILE (MMS) USE DURING AND UP TO 2 HOURS POST MATCH. FOR MORE INFORMATION CONTACT DFL
Bundesliga FC Köln Trainer Stale SolbakkenPicha: Reuters

Frank Schaefer alirea Ijumaa asubuhi kufanya maandalizi ya mchuano mkali Jumapili dhidi ya mahasimu wa jimbo la Rhein Borussia Moenchengladbach. Schaefer mwenye umri wa miaka 48 aliondoka klabu ya Cologne mwezi Aprili mwaka uliopita wakati klabu hiyo iking'ang'ana kuepuka shoka la kushushwa ngazi kutoka ligi kuu.

Cologne kwa sasa iko katika eneo la kushushwa daraja. Kichapo cha magoli manne kwa sifuri siku ya Jumanne ndicho kilichokuwa cha mwisho kwa Solbakken mwenye umri wa miaka 44 ambaye sasa ni kocha wa nane wa Bundesligha kuonyeshwa mlango msimu huu.

Mshambuliaji wa klabu ya Hanover 96 Mame Biram Doiuf amefutiliwa mbali kushiriki michuano minne iliyosalia ya ligi msimu huu kutokana na jeraha la kifundo cha mguu alilopata katika mechi waliyoshinda magoli mawili kwa sifuri dhidi ya VfL Wolfsburg Jumatano iliyopita.

Mame Biram Diouf amenawiri tangu alipojiunga na Hanover msimu huu
Mame Biram Diouf amenawiri tangu alipojiunga na Hanover msimu huuPicha: Reuters

Mshambulizi hiyo raia wa Senegal amejiweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshambuliaji nambari moja wa klabu hiyo tangu alipowasili akitokea Man United, na amefunga magoli sita ya Bundesliga na manne katika Ligi ya Ulaya Europa League. Hannover iko katika nafasi ya saba na alama 44 na inapambana kujipa fursa ya kushiriki dimba la Europa League tena msimu ujao.

David Rudisha ajiandaa kwa Olimpiki

Mshikilizi wa rekodi ya mbio za mita 800 ulimwenguni Mkenya David Rudisha anapanga kutimka mbio zisizozidi tatu kabla ya kushiriki katika mshindano ya Olimpiki jijini London, akianza na mashindano ya Diamond League kule Doha Qatar mwezi ujao wa Mei. Rudisha anapigiwa upatu kuongeza taji la Olimpiki kwa taji lake la ulimwengu aliloshinda kule Daegu Mwaka uliopita.

Hata hivyo Rudisha mwenye umri wa miaka 23, anasema mfumo wake wa kukimbia kutoka mbele ya wapinzani unafanya kuwa vigumu kwake kuendeleza ushindani wake.

David Rudisha alikosa kushiriki mashindano ya Olimpiki jijini Beijing mwaka wa 2008 kutokana na jeraha la kifundo cha mguu
David Rudisha alikosa kushiriki mashindano ya Olimpiki jijini Beijing mwaka wa 2008 kutokana na jeraha la kifundo cha mguuPicha: AP

Na mwanariadha wa mbio za masafa mafupi Majamaica Usain Bolt atafanya maandalizi yake ya Olimpiki kwa kushiriki mbio za mita 200 kule Monte Carlo, tarehe 20 Julai.

Hayo ni kwa mujibu wa chama cha riadha ulimwenguni IAAF. IAAF imesema Bolt amethibitisha kushiriki mbio hizo zza Herculis ambazo ni sehemu ya msururu wa mashindano ya Diamond League.

Pia atakimbia mbio za Diamnond League kule Rome tarehe 31 Mei na Oslo tarehe 7 Juni. Botl alishinda mbio za mita 100, 200 mita 100 wanariadha wanne kupokezana vijiti katika muda wa rekodi ya ulimwengu wakati wa mashindano ya Olimpiki kule Beijing mwaka wa 2008 na analenga kuyatetea mataji hayo katika mashindano ya Olimpiki London.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/Reuters/AP

Mhariri: Abdul-Rahman Mohamed