1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Asili na mazingiraUmoja wa Falme za Kiarabu

COP28 yafikia makubaliano kuachana na nishati za visukuku

13 Desemba 2023

Wawakilishi kutoka takriban nchi 200 wanaoshiriki mkutano wa kilele wa kimataifa wa Mazingira COP28 mjini Dubai, wamekubaliana leo kuanza kupunguza matumizi ya nishati za visukuku, ili kuepusha madhara ya tabia nchi.

https://p.dw.com/p/4a6Jy
Washiriki wa mkutano wa COP28 mjini Dubai
Washiriki wa mkutano wa COP28 wakufurahia kupatikana makubaliano.Picha: Amr Alfiky/REUTERS

Makubaliano hayo ni ya kwanza ya aina yake na yanaashiria mwanzo wa mwisho wa enzi ya matumizi ya mafuta.

Makubaliano hayo yametangazwa na Mkuu wa shirika la kitaifa la mafuta katika Umoja wa Falme za Kiarabu Sultan Al Jaber ambaye ndiye rais wa mkutano huo mwaka huu.

Makubaliano hayo yanakusudia kutuma ishara yenye nguvu kwa wawekezaji na watunga sera kwamba dunia sasa imeungana kuachana na mafuta, jambo ambalo wanasayansi wanasema ni tumaini bora la mwisho kuzuia janga la hali ya hewa.