1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Corona yaendea kuitikisa dunia

27 Desemba 2022

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida ametangaza kwamba Japan itaimarisha udhibiti wa Covid-19 mpakani kwa kuzingatia vipimo miongoni mwa wageni wote wanaoingia kutoka China.

https://p.dw.com/p/4LSv1
Japan Neue nationale Sicherheitsstrategie
Picha: David Mareuil/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida ametangaza kwamba Japan itaimarisha udhibiti wa Covid-19 mpakani kwa kuzingatia vipimo miongoni mwa wageni wote wanaoingia kutoka China. Kauli hii inajiri baada ya Chinakuondoa vikwazo vya kudhibiti maambukizo. Na wataalam wa virusi nchini Ujerumani wanasema Corona inaweza kuzingatiwa sasa kama ugonjwa wa kawaida.

soma Shanghai yakabiliwa na ongezeko la maambukizi ya Corona

Akitoa maoni yake katika gazeti la Tagesspiegel dakrari wa virusi katika Hospitali ya Chuo kikuu ya Berlin's Charité nchini Ujerumani Christian Drosten amesema baada ya majira ya baridi msimu huu kinga ya watu itaimarika zaidi na kustahamili virusi hivyo ambavyo vilikua na athari ndogo wakati wa msimu wa kiasi.

Akijibu matamshi ya Drosten, Waziri wa Sheria Marco Buschmann alitaka hatua zote za vikwazo ziruhusiwe kuondolewa. Kwa upande wake daktari wa wagonjwa mahututi Christian Karagiannidis, ambaye pia ni mjumbe wa baraza la wataalam la Covid-19 la Ujerumani, alisema janga hilo huenda likaisha baada ya majira ya baridi, akitilia mkazo kwamba kinga ya idadi ya watu imeimarika na kuna na wagonjwa wachache sana wa Covid-19 katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Kwa upande mwengine makampuni yamekaribisha uamuzi wa China wa kusitisha karantini kwa wasafiri kutoka nje ya nchi kama hatua muhimu ya kufufua shughuli za biashara zilizodorora, huku Japan hii leo ikitangaza vikwazo kwa wageni wanaoingia nchini humo wakati maambukizo yakiongezeka.

Waziri mkuu Kishida amesema udhibiti wa dharura wa mpaka utawekwa kwa wasafiri kutoka China kutokana na kuongezeka kwa idadi ya kesi mpya za corona:

"Kuna tofauti kubwa kati ya taarifa kutoka serikali kuu na serikali za mitaa, na taarifa tofauti kutoka Beijing na sekta binafsi. Hali hiyo imezua wasiwasi nchini Japani.”

Kulegezwa kwa vizuizi

China Corona-Pandemie | Peking
Picha: Noel Celis/AFP/Getty Images

Licha ya milipuko kuenea na kutatiza rasilimali za matibabu na kuvuruga biashara, China imesema kwamba abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi hawatalazimika tena kuwekwa karantini kuanzia Januari tarehe 8, lakini bado matokeo ya vipimo vya corona ndani ya masaa 48 kabla ya kusafiri na barakoa ndani ya ndege bado zinahitajika.

China imejiunga na nchi nyengine katika kutibu kesi badala ya kujaribu kukomesha maambukizi ya virusi kwa kuondoa au kurahisisha ya sheria kupima, inapojaribu kuboresha uchumi ulioporomaka. Hata hivyo mabadiliko hayo yamejaza hospitali kwa wagonjwa wa homa kali namatatizo ya kupumu.

Wataalam wametabiri vifo milioni 1 hadi 2 nchini China kufikia mwisho wa 2023.

Wiki iliyopita India pia iliamuru upimaji wa COVID-19 kwa wasafiri kutoka China, Japan, Hong Kong, Korea Kusini na Thailand, na kuagiza karantini kwa walio na dalili au kupimwa kuwa na virusi hivyo.