Nchini Tanzania, kuna ishara ya wazi ya kuwepo mgawanyiko ndani ya chama tawala nchini humo CCM, na hasa baada ya kuibuka mtu anaejitambulisha kuwa mwanaharakati huru, Cyprian Musiba na kuwashambulia viongozi waandamizi walio madarakani na wastaafu kwa kuwahusisha na tuhuma za kudhoofisha chama na serikali ya sasa ya chama hicho. Sudi Mnette amezungumza na Cyprian Musiba.