Dalili za Ebola
5 Desemba 2014Matangazo
Muda wa kupevuka kwa virusi vya Ebola, yaani wakati mtu anapoambukizwa hadi dalili za ugonjwa huo zinapoanza kuonekana, ni kati ya siku mbili hadi 21. Mara nyingi dalili hizi huanza kuonekana kati ya siku ya nane hadi ya kumi baada ya kuambukizwa, zikijidhihirisha kama dalili za malaria au homa.
- Homa
- Kichefuchefu na kutapika
- Kuharisha
- Vidonda vya koo
- Kuumwa kichwa
- Maumivu ya misuli
- Kusumbuliwa na tumbo
- Kuchoka
- Kukosa hamu ya kula
Dalili hizi zinaweza kujitokeza zote kwa pamoja, ingawa mgonjwa anaweza kuwa na dalili moja au mbili kati ya hizi. Dalili zinaweza kujitokeza siku ya tano baada ya mtu kuona dalili za kwanza za ugonjwa huu, na mgonjwa anaweza pia kuanza kutokwa na damu kupitia tundu za mwili, kama vile mdomoni, puani na sehemu za siri.