1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUlaya

Dalili zaonesha uchumi wa Ujerumani utaboreka 2024

20 Novemba 2023

Benki kuu ya Ujerumani imesema uchumi wa Ujerumani unatarajiwa kupungua tena katika robo mwaka na kuimarika kwake kutakuwa kugumu, licha ya kuwepo dadlili kwamba hali inaweza kuboreka mapema mwaka ujao.

https://p.dw.com/p/4ZEfH
Kiongozi | Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz (SPD)
Kiongozi | Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz (SPD)Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Ujerumani ambayo kwa sasa inapitia kipindi cha kushuka kwa shughuli za uchumi, imekuwa miongoni mwa mataifa yaliyo na uchumi dhaifu barani Ulaya mwaka huu huku kupanda kwa bei ya nishati na viwango vya juu vya riba vikichangia hali hiyo.

Taarifa ya Benki hiyo imesema uchumi wa Ujerumani unatarajiwa kuimarika tena pole pole, kufuatia kutetereka kidogo tangu kuanza kwa vita kwa Urusi nchini Ukraine.

Soma pia:Ujerumani yaunga mkono Nigeria kuwa kwenye G20

Ujerumani ilirekodiukuaji wa uchumiwa robo mwaka mara moja tu mwaka huu, na viashiria katika miezi mitatu ya mwisho wa mwaka vinaonesha mwelekeo wa kuzidi kushuka.