DARFUR: Annan alitembelea jimbo la mgogoro Darfur
28 Mei 2005Matangazo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan hii leo analitembelea eneo la mgogoro la Darfur,kama sehemu ya ziara yake ya siku tatu nchini Sudan.Lengo la ziara ya Annan ni kuimarisha juhudi za usalama na misaada ya kiutu katika jimbo la Darfur.Baada ya kuwa na majadiliano pamoja na serikali ya Sudan mjini Khartoum,Annan alielekea katika jimbo la Darfur akitaraji kuitembelea kambi kubwa kabisa ya wakimbizi.Zaidi ya watu laki moja na themanini elfu wameuawa Darfur na kiasi ya milioni mbili wengine wamelazimika kuhama makwao.Madola fadhili kwenye mkutano uliofanywa wiki hii katika mji mkuu wa Ethiopia,Addis Ababa,yaliahidi kutoa msaada wa Dola milioni kadhaa kwa tume ya Umoja wa Afrika inayosimamia usitishaji wa mapigano huko Darfur.