1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DARFUR. Umoja wa Afrika kuongeza wanjeshi maradufu.

29 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFIH

Umoja wa nchi za Afrika umepitisha azimio la kuongeza maradufu idadi ya walinda amani katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan kufikia mwezi septemba

Kufikia wakati huo Umoja wa Afrika unatarajia kuwepo kwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika wengi wao kutoka Kenya, Nigeria na Rwanda ili kuwalinda wanavijiji walioshambuliwa na vikundi haramu kwa miaka miwili iliyopita na vile vile kufanikisha mpango wa kusalimisha silaha.

Azimio hilo la Umoja wa nchi za Afrika linafuatia ahadi iliyo tolewa na wanachama wa NATO la kuusaidia Umoja wa Afrika ili kufanikisha lengo hilo kwa kutoa msaada katika nyanja za utaratibu wa ugavi na usafiri.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffie Annan amesema kuwa wakimbizi wapatao millioni mbili bado wanakabiliwa na tisho la kushambuliwa.