1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAVOS: Makubaliano ya biashara duniani ni muhimu

27 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXS

Viongozi wa kisiasa na uchumi wanaendelea na majadiliano yao katika Kongamano la Kiuchumi Duniani mjini Davos,Uswissi.Pembezoni mwa kongamano hilo,mawaziri kutoka nchi mbali mbali duniani wanakutana leo hii kuchunguza ikiwa wataweza kuyafufua mazungumzo ya utandawazi yaliyokwama.Majadiliano kuhusu biashara duniani yaliahirishwa mwaka jana kwa sababu ya tofauti zilizokuwepo hasa kuhusu siasa nyeti za biashara ya kilimo.Ingawa pande zote zinatazamiwa kujitolea,hakuna matumaini ya kupata hatua kamili za kuanzisha majadiliano.Hapo awali,maafisa 65 walio na usemi mkubwa katika sekta ya biashara duniani,walionya kuwa ukuaji wa uchumi duniani utahatarishwa,ikiwa makubaliano mapya ya biashara hayatopatikana.