DAVOS: Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, ataka Afrika izingatiwe.
27 Januari 2007Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, amesema Afrika itaathirika kwa kiasi kikubwa iwapo mwelekeo wa uchumi wa dunia hautazingatiwa ipasavyo.
Waziri Mkuu, Tony Blair, alikuwa akizungumza kwenye kikao cha jopo la mkutano wa dunia wa kiuchumi, World Economic Forum, mjini Davos, Uswisi.
Rais wa Liberia, Ellen Sirleaf Johnson na Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki waliunga mkono wito wa Tony Blair wa kuongeza msaada kwa bara la Afrika.
Mwanamuziki wa bendi ya U2, Paul David Hewson maarufu kwa jina Bono, alisema mataifa yaliyostawi bado hayajatilia maanani ipasavyo wazo la kuisadia Afrika.
Mwasisi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates, ambaye wakfu wake unatoa msaada wa chanjo kwa mataifa yanayoendelea, alisema ana matumaini makubwa ya uwezekano wa kumaliza maradhi yanayowakabili watoto barani Afrika.