1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Demokrasia zaidi ni suluhisho pekee Pakistan

T.Bärthlein - (P.Martin)18 Februari 2009

Mwaka mmoja baada ya demokrasia kurejea nchini Pakistan hali ya kutoridhika imezidi nchini humo,kwani chini ya utawala wa kiraia,makundi ya kigaidi kama Taliban yameweza kueneza ushawishi wake kuliko hapo awali.

https://p.dw.com/p/GwxG
A handout picture released by Associated Press of Pakistan (APP) on 20 September 2008 shows widower of slain former Prime Minister Benazir Bhutto and newly elected Pakistan's President Asif Ali Zardari, as he speaks to the Parliamentarians in Islamabad Pakistan. Pakistan's new President Asif Ali Zardari said on September 20, his government would not allow any foreign nation to carry out attacks inside the country, a reference made to the recent US missile attacks in Pakistan's border areas near Afghanistan. Asif Ali Zardari was addressing the joint session of the parliament for the first time after taking oath of the office of the President. EPA/ASSOCIATED PRESS OF PAKISTAN HANDOUT EDITORIAL USE ONLY +++(c) dpa - Report++
Rais wa Pakistan,Asif Ali Zardari.Picha: pa / dpa

Pakistan,juma hili imekosolewa tena na jumuiya ya kimataifa-safari hii ni kwa sababu ya kuanzishwa sheria za Kiislamu katika Bonde la Swat.Ni sawa kuikosoa kwani makubaliano yaliyopatikana kati ya serikali ya wilaya na wanamgambo wenye itikadi kali ni ishara ya kusalim amri kwa Wataliban ambao kwa kweli hudhibiti eneo la Kaskazini-Maghairibi ya Pakistan.Bila shaka wanamgambo hao sasa wamepata moyo kuendeleza mbinu zao za kigaidi katika maeneo mengine ili kufikia malengo yao.

Kwa upande mwingine mtu lazima akiri kuwa ni rahisi kukosoa ukiwa mbali. Lakini kuna chaguo gani jingine mbali na mkataba huo na Taliban? Operesheni za kijeshi hazikuleta ufumbuzi katika kanda hiyo na hata maeneo mengine nchini Pakistan.Ni dhahiri kuwa majeshi yameshindwa, isipokuwa kwa mafanikio ya hapa na pale kuzuia uasi.Majeshi hayo hayana nguvu za kuweza kudhibiti maeneo hayo.Isitoshe,hatua kali kupita kiasi zinazochukuliwa dhidi ya raia husababisha wakaazi hao kuwa wafuasi wa Taliban.

Itakuwa kosa hivi sasa kutilia shaka demokrasia na kutamani siku za utawala wa kidikteta chini ya Jenerali Musharraf.Tatizo la Pakistan si kwamba jamii inafuata itikadi kali.Kwani ingekuwa hivyo,basi vyama vyenye itikadi kali za Kiislamu vingeshinda uchaguzi huru uliofanywa nchini humo mwaka mmoja uliopita.Kinyume na hivyo makundi hayo yalishindwa vibaya. Tatizo mojawapo kuu ni nguvu za jeshi na idara ya upelelezi,zinazozidi kuongezeka tangu miongo kadhaa na pia uhusiano wake na makundi yenye itikadi kali za Kiislamu.

Kwani jeshi lilisaidia kuviimarisha vyama vya Kiislamu katika jitahada ya kuvizuia vyama vikubwa vya kidemokrasia. Makundi ya wanamgambo yalisaidiwa kupigana jihadi nchini Afghanistan na katika jimbo la Kashmir kwa madai kuwa ni kwa maslahi ya Pakistan.

Lakini hapa lazima isisitizwe kuwa nchi za Magharibi pia zinabeba sehemu ya makosa.Kwani bila ya msaada uliotolewa kwa dikteta Zia ul-Haq wakati wa vita dhidi ya Soviet Union ya zamani nchini Afghanistan na Pervez Musharraf baada ya mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001,jeshi la Pakistan lisingeweza kuwa na nguvu kama hivyo.

Lakini suluhisho pekee ni demokrasia.Pakistan yenyewe itajitafutia njia ya kumaliza mgogoro wake na Wataliban kwani wengi wa wakaazi wa Pakistan hawataki kutawaliwa na Wataliban.Lakini hakuna anaewauliza maoni yao.