DHAKA: Kimbunga SIDR kimesababisha hasara ya maisha na mali
16 Novemba 2007Matangazo
Hadi watu 200 wameuawa kusini-magharibi ya Bangladesh,baada ya kimbunga Sidr kuvuma katika eneo hilo kwa kasi ya hadi kilomita 240 kwa saa. Serikali ina hofu kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu bado watu wengi wanakosekana.Kimbunga hicho kimesababisha mvua na mafuriko makubwa na maelfu ya nyumba na vibanda vimeteketezwa.
Siku ya Alkhamisi kiasi ya watu 350,000 walihamishwa maeneo mengine.Kimbunga hicho sasa kinaelekea mji mkuu Dhaka ulio kaskazini mwa nchi.Kimbunga Sidr kimesababisha maafa makubwa nchini India vile vile.