Djokovic ashinda kesi dhidi ya Australia
10 Januari 2022Matangazo
Mawakili wa Djokovic walisema kwamba ana udhuru wa kimatibabu baada ya kuugua virusi vya corona hivyo hastahili kuchomwa chanjo jambo ambalo serikali ya Australia ilikataa na kumzuia tangu wiki iliyopita.
Lakini sasa mahakama hiyo imetoa amri ya kuachiwa kwa mchezaji huyo wa Tennis ila waziri wa uhamiaji wa Australia Alex hawke anatafakari iwapo aifutilie mbali visa ya Djokovic kwani kisheria anaweza kufanya hivyo licha ya amri ya mahakama, jambo litakalomaanisha kwamba Djokovic atakuwa na marufuku ya kuingia Australia kwa miaka mitatu.
Wachezaji wenzake wameanza kumuunga mkono kwa mfano kufuatia uamuzi huo wa mahakama Rafael Nadal amesema kwamba Djokovic sasa anastahili kuruhusiwa ashirike kombe la Australian Open.