1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund waendelea kupepea kileleni

27 Machi 2012

Mabingwa washikilizi wa ligi ya soka Ujerumani Bundesliga, Borussia Dortmund walisalia kileleni na tofauti ya alama tano baada ya kutoka nyuma na kuwasambaratisha FC Cologne magoli sita kwa moja.

https://p.dw.com/p/14SRn
Borussia Dortmund's Shinji Kagawa celebrates a goal against Cologne during the German first division Bundesliga soccer match in Cologne March 25, 2012. REUTERS/Ina Fassbender (GERMANY - Tags: SPORT SOCCER) DFL LIMITS USE OF IMAGES ON THE INTERNET TO 15 PICTURES DURING THE MATCH AND, PROHIBITS MOBILE (MMS) USE DURING AND UP TO 2 HOURS POST MATCH. FOR MORE INFORMATION CONTACT DFL
Fußball Bundesliga, 27. SpieltagPicha: Reuters

Milivoje Novakovic aliwaweka Cologne kifua mbele lakini Lukasz Pisczczek alisawazisha. Kisha katika kipindi cha pili wageni Dortmund walifanya mashambulizi makali huku magoli mawili yake Mjapan Shinji Kagawa na moja kila mmoja kutoka kwa wachezaji Robert Lewandowski, Ilkay Gundogan na Ivan Perisic yakimaliza kazi.

Nambari mbili Bayern Munich ambao wamekuwa wakiongeza shinikizo kupitia idadi ya magoli katika mechi za hivi karibuni, walilazimika kuridhika na ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Hannover 96. Toni Kroos na Mario Gomez ndio walioifungia Bayern huku Didier Ya Konan akiwafutia machozi Hannover.

Vita vya Man United na Man City

Katika ligi Premier League ya Uingereza, Manchester United walikuwa na wikendi ya furaha hata ingawa hawakuwa uwanjani, baada ya mahasimu wao wa taji Manchester City kumudu tu sare ya bao moja nyumbani kwa Stoke City. Hivyo City wanaongoza tu ligi wakiwa na faida ya magoli  lakini hii leo usiku United watakuwa na fursa ya kuongoza kwa tofauti ya alama tatu ikiwa watawashinda Fulham uwanjani Old Traford.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amewaongoza vijana wake kusajili matokeo bora hivi karibuni
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amewaongoza vijana wake kusajili matokeo bora hivi karibuniPicha: AP

Vita vya kuwania ligi ya mabingwa msimu ujao vinaonekana kushindwa na Arsenal, baada ya kusajili ushindi wa kuridhisha wa magoli matatu kwa mawili dhidi ya Aston Villa.

Huo ulikuwa ushindi wao wa saba mfululizo na ukawasongeza alama tatu juu ya Tottenham Hotspur iliyotoka sare ya bila kufungana na Chelsea ambao wako nafasi ya tano. Mchezaji wa Newcastle raia wa Senegal Papiss demba Cisse alifunga magoli mawili na kuwasaidia Newcastle kusajili ushindi wa magoli matatu kwa moja dhidi ya Westbromwich Albion.

Ushindi huo uliwaweka nafasi sawa na Chelsea ijapokuwa na tofauti ya magoli. Wigan Athletic walishinda kwa mara ya kwanza uwanjani Anfield kwa kuwafunga Liverpool magoli mawili kwa moja.

Muamba alizirai wakati wa mchuano wa kombe la FA dhidi ya Tottenham Hotspurs
Muamba alizirai wakati wa mchuano wa kombe la FA dhidi ya Tottenham HotspursPicha: Reuters

Muamba aliwatazama wenzake

Na kuhusiana na hali ya afya ya Kiungo wa Bolton Fabrice Muamba ni kuwa aliwatazama wachezaji wenzake wa Bolton wakicheza dhidi ya mahasimu wao Blackburn Rovers kupitia televisheni lakini alisinzia na kulala kabla ya mechi kukamilika.

Muamba alisinzia wakati Bolton ilikuwa ikiongoza kwa magoli mawili kwa sifuri. Meneja wa Bolton Owen Coyle alisema Fabrice anaweza kuwatambua watu na kujibu maswali.

Kiungo huyo hata hivyo angali katika chumba cha wagonjwa mahututi. Mchuano uliopangwa upya kati ya Tottenham na Bolton wa kombe la FA utachezwa kesho Jumanne katika uga wa White Hart Lane na kundi la wachezaji wa Bolton litamtembelea Muamba hospitalini kabla ya pambano hilo.

Ligi ya mabingwa Ulaya

Mechi za robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya zinarejea kesho Jumanne ambapo Benfica itaikaribisha Chelsea nchini Ureno, huku APOEL Nicosia ikiwa mwenyeji wa Real Madrid nchini Cyprus. Beki Branislav Ivanovic anatarajiwa kurejea baada ya kukosa mchuano dhidi ya Tottenham. Roberto di Matteo ataamua ikiwa atamwita kikosini David Luiz kushirikiana na John Terry katika safu ya ulinzi au asalie na Gary Cahill.

Chelsea inakabiliwa na wakati mgumu katika ligi ya Uingereza
Chelsea inakabiliwa na wakati mgumu katika ligi ya UingerezaPicha: dapd

David Luiz na kiungo Ramires wote ni wachezaji wa zamani wa Benfica. Fernando Torres huenda akaitwa kuchukua mahala pa Didire Drogba aliyeanza katika mchuano wa Spurs.

Jumatano, AC Milan itakuwa nyumbani San Siro kucheza dhidi ya mabingwa watetezi Barcelona. Marseille itawakaribisha Bayern Munich nchini Ufaransa.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters

Mhariri:Yusuf Saumu