1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund yapunguza pengo na Bayern

9 Novemba 2015

Borussia Dortmund walijigamba kwa kuwashinda Schalke katika mchuano wa Ruhr derby magoli matatu kwa mawili na hivyo kupunguza pengo Kati yao na viongozi wa wa ligi Bayern Munich

https://p.dw.com/p/1H2Q3
Fußball Bundesliga 12. Spieltag Borussia Dortmund - FC Schalke 04
Picha: picture-alliance/dpa/B. Thissen

Baada ya kushuhudia Bayern Munich wakipanua pengo lao kwa point inane kileleni mwa Bundesliga kwa kuwazaba Stuttgart mabao manne kwa sifuri siku ya Jumamosi, labda haukuwa wakati bora kwa Borussia Dortmund kuwakaribisha Schalke uwanjani Signal Iduna Park jana Jumapili kwa mchuano mkali wa Ruhr derby. Na kama tu ilivyotarajiwa, kulikuwa na makabiliano makali huku watu wakipigwa viatu kutoka mwanzo, lakini pia kulikuwa na kandanda safi lililochezwa.

Mwishowe, Dortmund iliibuka kidedea kwa kuifunga Schalke mabao matatu kwa mawili ikiwa ni ushindi wao wa nane mfululizo kazika mashindano yote, na hivyo wakapunguza pengo baina yao na viongozi Bayern hadi pointi tano. Schalke wanasalia katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi lakini sasa hawajashinda katika mechi sita.

Bayern München PK Josep Guardiola
Hatma ya Guardiola kuamuliwa baada ya KrismasiPicha: Getty Images/Bongarts/A. Pretty

Safu ya mashambulizi ya miamba wa Bavaria Bayern Munich iliwahangaisha Suttgart wakiongozwa na Arjen Robben, Douglas Costa, Robert Lewandoskwi na Thomas Müller kwa kuwafunga nne bila. Bayern wameigeuza Allianz Arena kuwa ngome kwa kufunga magoli 28 katika mechi zao sita za mwisho nyumbani, na kufungwa tatu tu na sasa wana pointi 34 kati ya 36, timu pekee ya bundesliga ambayo haijashindwa mchuano wowote kufikia sasa.

Lakini suali ni, je, kocha Pep Guardiola anaondoka au haondoki? Mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummennigge ameahidi zawadi ya Krismasi. Amesema hatima ya Bayern itaamuliwa hivi karibuni wakati wa kipindi cha mapumziko ya msimu wa baridi. Mkataba wa Guardiola unakabilika mwishoni mwa msimu huu, na anaendelea kuhusishwa na uvumi wa kuhamia ligi kuu ya England.

Augsburg inasalia katika nafasi ya mkia baada ya kichaponcha mbili moja dhidi ya Werder Bremen. Makamu bingwa wa msimu uliopita Wolfsburg wako nyuma ya Bayern na tofauti ya pointi 13 baada ya kuchabangwa mbili sifuri na Mainz. Bayer Leverkusen pia walizabwa mbili moja na majirani Cologne katika mchuano wa Rhine derby. Hoffenheim inasalia ya pili kutoka nyuma baada ya kutoka sare ya bila bila na Eintracht Frankfurt wakati Hamburg ilitoka sare ya moja moja na Darmstadt. Borussia Moenchengladbach ilitoka sare ya bila kufungana na Ingolstadt. Hertha Berlin ilipata ushindi wa tatu moja dhidi ya Hanover na kuchukua nafasi ya nne kwenye ligi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu